Huduma za Usafiri wa Treni kutoka Dar es Salaam kuelekea Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Katavi, Kigoma na njia ya Kaskazini kuelekea Tanga imeendelea kusitishwa, ikielezwa miundombinu imeharibiwa na Mvua
Taarifa ya Shirika la Reli Tanzania (#TRC) imeeleza kuna uharibifu wa miundombinu ya Reli kati ya Stesheni ya Morogoro na Mazimbu, Munisagara na Mzaganza Wilaya ya Kilosa (Morogoro) na Godegode na Gulwe Wilaya ya Mpwapwa (Dodoma) na eneo la Wami, Ruvu (Pwani) na Mkalamo (Tanga)
Aidha, taarifa imeeleza kuwa Wahandisi wa TRC wanaendelea na matengenezo maeneo yaliyoathiriwa na Mvua zinazoendelea na taarifa ya huduma kurejea itatolewa baada ya kukamilika kwa matengenezo ya miundombinu hiyo