Huu Hapa Ndio Uwanja Mkubwa Zaidi Kwenye Mashindano ya AFCON 2024

Huu Hapa Ndio Uwanja Mkubwa Zaidi Kwenye Mashindano ya AFCON 2024


Kuna viwanja sita [6] ambavyo vinatumika kwenye michuano ya AFCON 2023 ambayo inaendelea kwenye miji mikubwa mitano [5] hapa nchini Ivory Coast.


Kitu kizuri na cha kupendeza ni namna ambavyo Serikali ya Ivory Coast ilivyoamua kuvipa viwanja hivyo majina ya watu mashuhuli waliolitumia taifa hilo katika sekta tofautitofauti kama sehemu ya kukumbuka na kuenzi kile walichokifanya.


Viwanja vitano [5] kati ya sita [6] vimepewa majina ya watu, hapa nakuletea orodha ya viwanja vyote sita [6] na sababu ya kupewa jina husika.

Alassane Ouattara Stadium

Uwanja huu wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 60,000 walioketi upo kwenye jiji la Abidjan sehemu ambayo ndio kitovu cha uchumi wa Ivory Coast.

Awali uwanja huu ulikuwa unafahamika kwa jina la Olympic Stadium of Epimbe lakini baadae ukabadilishwa jina na kuitwa Alassane Ouattara Stadium [Jina la Rais wa sasa aliyepo madarakani].

Huu ndio uwanja mkubwa zaidi kati ya viwanja sita vinavyotumika kwa ajili ya miachuano ya AFCON 2023, ulifunguliwa rasmi Oktoba 3, 2020.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad