Kenya: AirBnB zaruhusiwa kurekodi matukio kukithiri kwa mauaji

 

Kenya: AirBnB zaruhusiwa kurekodi matukio kukithiri kwa mauaji

Kutokana na kuongezeka kwa ripoti za vitendo vya uhalifu ikiwa ni pamoja na kesi za mauaji, katika nyumba za makazi maarufu kama (AirBnB) na Hoteli Mamlaka ya Udhibiti wa Taarifa Binafsi imetoa maagizo yanayolenga kuzuia vitendo hivyo na kuhakikisha usalama wa wakazi na wageni


Mamlaka hiyo imewataka watoa huduma wote wanaotoa huduma kwenye nyumba za wageni, hoteli, na AirBnB kuzingatia cha 48 cha Sheria ya Taarifa Binafsi ya nchi hiyo kwa Kurekodi na kutunza kumbukumbu za utambulisho wa wageni, Kudhibiti na kurekodi muda wa kuingia na kutoka kwa wageni na pia Kukusanya na kuhifadhi kwa muda Vitambulisho vya wageni


Usalama wa AirBnB nchini Kenya umekuwa mashakani katika siku za hivi Karibuni baada ya Matukio ya Mauaji ya Kinyama ya Wateja akiwemo Mwanamitandao #ScarletWahu na Mwanamke mmoja ambaye aliuawa kisha mwili wake kukatwa vipande na kuwekwa kwenye ndoo ya taka huko Kasarani

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad