KIPA Onana Akwea Pipa, Aiwahi Wolves



Nyanda wa Manchester United na Cameroon, Andre Onana yupo safarini kurejea England tayari kwa kuendelea na majukumu yake na Mashetani Wekundu baada ya Cameroon kusukumizwa nje ya AFCON 2023.


Meneja wa Man United, Eric Ten Hag amethibitisha kuwa kipa huyo wa zamani wa Barcelona, Ajax na Inter Milan atakuwa sehemu ya kikosi chake kitakachoikabili Wolves siku ya Alhamisi.


Onana alikuwa sehemu ya kikosi cha Cameroon kilichofuzu hatua ya 16 bora ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2023 kabla ya kuondoshwa kwenye hatua hiyo kufuatia kipigo cha 2-0 dhidi ya Nigeria.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad