Beki huyo ni sehemu ya wachezaji wanaounda kikosi cha Timu ya Taifa ya DR Congo kilichotinga Robo Fainali kwa kuifunga Misri katika mchezo wa Hatua ya 16 bora kwa njia ya Penati.
Inonga akiwa katika michuano hiyo, nchini lvory Coast tetesi zinasema kuwa klabu ya RS Berkane ya chini Morocco imeonyesha nia kubwa ya kumuhitaji beki huyo anayeunda kikosi cha kwanza cha DR Congo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Simba SC, Benchikha amezuia beki huyo kuuzwa katika klabu yoyote huku akiuonba uongozi umuongezee mkataba mwingine wa kuendelea kubakia klabuni hapo.
Mtoa taarifa hizo amesema kuzuia kuuzwa kwa beki huyo ni kutokana na kuwepo katika mipango yake ya muda mrefu ya kuendelea kubakia klabuni hapo ili kufanikisha malengo yake aliyoyatoa ya kubeba makombe yote wanayoshiriki kwa kuanzia msimu huu.
“Inonga ni kati ya wachezaji waliopo katika mipango ya muda mrefu ya kocha wetu Benchikha, ambaye amezuia kuuzwa kwa beki huyo katika msimu huu.
“Hivyo hatauzwa kwenda popote katika msimu huu, badala yake ataendelea kubakia hapa Simba SC kutokana na kiwango chake ambacha anacho hivi sasa.
“Pia wapo wachezaji wengine ambao kocha ameshauri kutoondoka klabuni hapo, huku akishinikiza kuwaongeza mikataba mingine,” aliserna mtoa taarifa huyo.
Akizungumzia hilo Meneja wa Habari na Mawasilano wa Simba, Ahmed Aly amesema kuwa: “Inonga yupo na ataendelea kuwepo Simba SC, kwani ni mchezaji mwenye mkataba wa kuendelea kuwepo hapa, ngumu kumuachia kwa sasa mchezaji aina ya Inonga.