Kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka barani Afrika Caf imemfungia kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Adel Amrouche mechi 8 kwa kutoa kauli ambazo zimetafsiriwa kama ni kauli za uchochezi.
Siku moja kabla ya mchezo wa kwanza dhidi ya Morocco kocha Adel aliwatuhumu Morocco kwamba wao ndio wanaouendesha mpira wa Afrika kwa kuamua wacheze muda gani, waamuzi wa mechi zao na kupanga ratiba za michezo yao.
Kauli hiyo ilikanushwa na TFF kupitia Rais Wallace Karia kuwa kauli hiyo ni ya kocha na sio ya TFF.
Chama cha soka cha Morocco kilipeleka malalamiko Caf kwa kauli hizo hali ambayo ililazimisha kamati ya nidhamu kukutana na kutoa adhabu ya kumfungia mechi 8 huku akipewa siku tatu za kukata rufaa.
Kwa kufungiwa kwa kocha Amrouche sasa ni wazi kocha Hemed Moroko na Juma Mgunda.