Kuhusu Kijana Kujirusha Bahati Kutoka Kwenye BOT Mamlaka Zanzibar Wafunguka



MAMLAKA YA USAFIRI BAHARINI ZANZIBAR YAKIRI KUPOKEA TAARIFA.

CCTV ZAONYESHA TUKIO LA KIJANA AKIJIRUSHA BAHARINI AKITOKEA KWENYE BOTI YA ZANZIBAR 3

Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri Bahari Zanzibar Shekha Ahmed Mohamed amekiri kupokea taarifa za kujirusha baharini kijana mmoja jina Mahmoud Mwalim Saleh ‘30’ wakati akiwa kwenye boti ya Zanzibar 3 iliyokua ikitokea Pemba kurejea Zanzibar

Tukio hilo limetokea majira ya saa 4:30 asubuhi wakati boti hiyo ikitokea Pemba na ilipofika eneo la Fungu Mayale ndipo kijana huyo alipojirusha

Boti hiyo ilizunguka maeneo hayo mara tatu kwaajili ya kufanya doria ya kumtafuta lakini haikufanikiwa kumuona, pia Kikosi cha KMKM kilifanya juhudi za kumtafuta lakini hakuonekana.

Mpaka sasa kijana huyo Bado hajaonekana licha ya mamlaka husika kufanya jitihada kumtafuta.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad