Kutokana na Mauaji Kuzidi Nchini Kwenye Nyumba za AirBnB, Kenya Watoa Sharti Hili Kwa AirBnB

Kutokana na Mauaji Kuzidi Nchini Kwenye Nyumba za AirBnB, Kenya Watoa Sharti Hili Kwa AirBnB


Kutokana na ongezeko la ripoti za uhalifu unaohusisha kesi za mauaji katika nyumba za makazi maarufu kama (AirBnB) na Hoteli, Mamlaka ya Udhibiti wa Taarifa Binafsi imetoa maagizo yanayolenga kuzuia vitendo hivyo na kuhakikisha usalama wa wakazi na wageni

Mamlaka hiyo imewataka watoa huduma wote kwenye nyumba za wageni, hoteli na AirBnB kuzingatia Sheria ya Taarifa Binafsi ya Nchi hiyo kwa Kurekodi na kutunza kumbukumbu za utambulisho wa wageni, kurekodi muda wa kuingia na kutoka kwa wageni na pia Kukusanya na kuhifadhi kwa muda Vitambulisho vya wageni

Usalama wa Wageni wanaotumia AirBnB nchini humo umekuwa mashakani katika siku za Karibuni baada ya Matukio ya Mauaji ya Wateja akiwemo Mwanamitandao #ScarletWahu na Mwanamke mwingine aliyeuawa na mwili wake kukatwa vipande na kuwekwa kwenye ndoo ya taka huko #Kasarani

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad