Mabasi ya Kilimanjaro Yafungiwa Kwa Kuzudisha NAULI na Kutotoa Risiti
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (#LATRA), Habibu Suluo ameagiza Mabasi yote ya Kampuni ya #KilimanjaroExpress kusitisha kutoa huduma kuanzia Januari 8, 2024 kutokana na kukiuka masharti ya leseni, ikiwamo kutotoa tiketi za kielektroniki na kuzidisha nauli kwa abiria, hadi pale itakapofanya Maboresho
Akizungumza baada ya ukaguzi wa kushtukiza katika Stendi ya #Magufuli pamoja na ofisi za #Shekilango, Suluo amesema, "Na leo tumelikamata Gari la Kampuni hii (Dar-Moshi-Arusha) likiwa limezidisha nauli kwa Abiria. Kila Abiria alilipishwa nauli tofauti. Tukawataka wawarejeshee nauli zao, wakakubali, lakini muda mfupi tumetoka kwenye Ofisi zao wakakataa kurejesha, eti mpaka Bosi wao aseme,"
Ameongeza, "Na hii siyo mara moja, wamekuwa wakifanya hivi mara nyingi na tumewaonya mara kwa mara na anaona kulipa faini ni kawaida kwake. Sasa sisi lengo letu ni kutaka wafuate Sheria na masharti ya leseni, watoe huduma bora na siyo kutoa faini. Na kama anaona kulipa faini ni kawaida kwake sisi hatuwezi kuvumilia"