Makonda Asimikwa Kuwa Chifu Msaidizi wa Hangaya


Makonda Asimikwa Kuwa Chifu Msaidizi wa Hangaya


Katibu wa NEC, Itikadi Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Paul Makonda, amesimikwa na Machifu wa Shinyanga kuwa “Nsumba Ntale” Kijana Mkuu ambaye atakuwa msaidizi wa Chifu Hangaya Rais Samia Suluhu Hassan.


Tukio hilo la kusimikwa Makonda limefanyika wakati alipowasili mkoani Shinyanga kwa ziara ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua, pamoja na kutoa maelekezo kwa viongozi wa Serikali na Chama ya kuwatumikia wananchi, likiongozwa na Chifu Njange Jidola wa Pili kwa niaba ya Machifu wote wa Mkoa huo.


Chifu Jidola akizungumza wakati wa kumismika Makonda kuwa Nsumba Ntale, amesema kazi yake kubwa itakuwa na kumsaidia Chifu Hangaya ambaye ni Rais Samia katika shughuli zake zote za kuwatumikia wananchi huku wakimpatia pia na jina la Mwijigejiwa lenye maana ya kwamba anayetegemewa sana.

“Baada ya kukusimika kuwa Nsomba Ntale sasa tuna kuvalisha shuka nyeusi ambayo ni ishala ya mawingu mazito yenye mvua na neema kwa wananchi, na hii shuka nyekundu na mkuki kwa ajili ya ulinzi wa chama na serikali, na mkufu wa huu wa simba ni ishara ya upendo,” amesema Chifu Jidola.


Naye Makonda ameshukuru Machifu kwa Kumsimika kuwa Nsomba Ntale na kuahidi kwamba hato waangusha bali atafanya kazi ya kumsaidia Chifu Hangaya, na hatokuwa na ushirika na watu waovu wa kuonea wanyonge katika Taifa hili


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad