Manara, Dulla Makabila wafika pabaya, njiwa wa kichawi anaswa!

 

Manara, Dulla Makabila wafika pabaya, njiwa wa kichawi anaswa!

Damu itamwagika mwaka huu! Vita kali ya maneno iliyopo kati ya Msanii wa Bongo Flena na Haji Manara imezidi kushika kasi na safari hii, ushirikina umehusika.


Hii muvi ilianza hivi, Manara baada ya kumchukuwa aliyekuwa mke wa Dulla Makabila mrembo kabisa Zaiylissa, Dulla alishusha bonge la songi la kumchana Zaiylissa pamoja na bwanake huyo mpya, msemaji wa zamani wa klabu ya Yanga, bwana Haji Sunday Manara. Kwenye songi hilo, Dulla amesikika akamchamba Zaiylissa kwa kutumia tafsida ya maneno.


Amemchamba kwamba alikuwa anamdangia akiwa ndani ya ndoa, amemchamba kuwa anapenda kutrendi hivyo anatoa siri hadi za ndani na kama haitoshi, hajui kupika duuuuuu!


Takirudi kwa Manara yeye akiwa kwenye press na Zaiylissa, mkewe mtarajiwa, alianza kwa kusema hataki kumpa Kiki Dulla lakini alipochokozwa zaidi na waandishi kwamba Dulla na washikaji zake wanazo video za utupu za bibie Zaiylissa, Manara aligeuka mbogo na kusema kama kweli wanazo hizo video waziachie ndio wanamjua yeye ni nani...


 Sasa Dulla naye kaibuka na jipya, anadai kuwa Manara kamtumia njiwa wa kishirikina nyumbani kwake na kwamba amegonga mwamba...


Dulla bhaana, eti anasema, njiwa huyo hajafua dafu kwani hakuna aliyeumwa hata homa nyumbani kwake hahaha hebu tucheke kidgo.


Anasema eti yeye anaijua michezo hiyo ya kishirikina na kilichobaki kwake ni kupaa na ungo tu...


Kwenye kipande hicho cha video ambacho kinasambaa mitandaoni, Rushaynah ambaye aliwahi kuwa mke wa Manara na kisha kuachana naye hakupitwa na sekeseke hilo akaamua kucomment kwenye post hiyo ya Dulla kwa kuabdika "Ila Abdallah kifupi Umeshindikana."

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad