Mangungu "Pesa Waliochanga Mashabiki wa Simba Kujenga Uwanja Ilitumika Kujenga Fensi"


Mangungu "Pesa Waliochanga Mashabiki wa Simba Kujenga Uwanja Ilitumika Kujenga Fensi"

“Simba imeshafanya mambo mengi makubwa, yaliyopita, yanayofanyika sasa na mengine yanakuja.”

“Sisi mliotupa dhamana tupo tayari kupokea maoni ambayo yataipeleka Simba mbele.”

“Lengo letu ni kujenga umoja. Mfano mtu anasema uwekezaji hauna faida wakati kabla ya uwekezaji mapato yalikuwa Tsh. 1.6 bilioni, mara baada ya uwekezaji yamepanda hadi Tsh. 6.9 bilioni. Afrika tulikuwa nafasi zaidi ya 80 kwenye ubora na sasa tupo nafasi ya saba. Tunataka ukosoaji wenye tija.”

“Kama mnakumbuka mlichanga pesa kwa ajili ya ujenzi wa uwanja na pesa ile ilitumika kujenga ukuta wa uwanja wa Bunju na pesa zingine zilitumika kuimarisha kambi ya timu.”

“Tujenge Simba imara kwa kizazi cha sasa na baadae. Tuendelee kushirikiana na naamini Mwenyezi Mungu atatutangulia. Mkutano umefunguliwa.”

Mwenyekiti wa Klabu, Murtaza Mangungu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad