Mchazaji Beki Kisiki Inonga Ajiwekea Rekodi AFCON


Beki kisiki wa Simba, Henock Inonga Baka amejitengeneza rekodi yake kwenye Fainali za Afcon, kwa kuwa mchezaji wa kwanza anayecheza Ligi Kuu Bara kufuzu robo fainali ya michuano hiyo.

Inonga aliweka rekodi hiyo baada ya ushindi wa timu ya taifa ya DR Congo wa penalti 8-7 dhidi ya Misri na kutinga robo fainali ikiwa ni mara ya 12 tangu ilipoanzishwa michuano hiyo mwaka 1957.

Inonga aliingia dakika ya 65 kwenye mchezo huo akichukua nafasi ya Dylan Batubinsika na alifunga mkwaju wa nane kati ya tisa iliyopiga DR Congo, huku mkwaju wa mwisho ukifungwa na kipa Lionel Mpasi –Nzau na kutinga hatua hiyo.

Mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Laurent Pokou (San Pedro) unaochukua mashabiki 2000, dakika 90 zilimalizika kwa sare ya bao 1-1 na kuongezwa nyingine 30, kabla ya kuamuliwa kwa mikwaju ya penalti tano kila moja.

Bao la DR Congo lilifungwa dakika ya 37 na Meshak Elia huku la Misri likifungwa na Mostapha Mohamed kwa penalti dakika ya 45+1.

Kwenye mikwaju ya penalti Misri ilipata mikwaju saba ikikosa miwili, huku DR Congo ikipata nane na kukosa mmoja.

Inonga alipiga penati ya nane kwa DR Congo ambayo kipa wa Misri, Mohamed Abou Gabal alishindwa kuupangua na kutinga wavuni.

Inonga anatarajiwa kuwepo kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya Guinea ya Ikweta, Ijumaa, Februari 2, kwenye Uwanja wa Alassane Ouattara, jijini Abidjan.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad