Mchezaji Jesus Moloko Afunguka Kutemwa Yanga,

Mchezaji Jesus Moloko Afunguka Kutemwa Yanga,


Muda mchache baada ya Mwanaspoti kuweka wazi kuachwa kwa winga, Jesus Moloko kuachwa na Yanga dirisha hili la usajili kupisha usajili mpya winga huyo amekiri hilo.


Yanga imeachana na winga huyo baada ya kuitumikia kwa misimu miwili hivyo ameungana na Wacongo wenzake Djuma Shaban, Yanick Bangala, Heritier Makambo, Chico Ushindi ambaye hakuweza kuendana na kasi ya Yanga na Fiston Mayele aliyeuzwa nje.


Akizungumza na Mwanaspoti, Moloko alisema ni kweli amemalizana na Yanga na anatarajia kuondoka nchini kesho kwenda Congo kwa ajili ya maisha mengine mapya ya soka.


"Ni kweli nimepewa barua ya kuachana na Yanga na natarajia kwenda Congo kesho nawashukuru viongozi na mashabiki wa timu hii kwa maisha niliyoishi nao nikiwa ndani ya timu hiyo;


"Nilikuwa na misimu mitatu mizuri na Yanga nimeishi vizuri na wachezaji wenzangu, viongozi na hata mashabiki nawatakia kila la kheri kwenye mashindano wanayoshiriki ndani na nje," alisema

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad