Mchezaji Victor Osimhen Ahofiwa Kutumia Dawa za Kuongeza Nguvu AFCON, Achukuliwa Vipimo



Mchezaji wa Kimataifa wa Nigeria, Victor Osimhen kufanyiwa vipimo ili kubaini kama alitumia dawa za kuongeza nguvu kwenye mchezo dhidi ya Cameroon katika hatua ya 16 bora ya michuano ya AFCON 2023.

Shirikisho la Soka Afrika walimchagua Osimhen baada ya ya mechi kufuatia kiwango bora dhidi ya Cameroon, kwa sababu alikimbia eneo kubwa na kukaba kwa mafanikio karibu kila eneo la uwanja.

Vipimo hivyo vitafanywa kabla ya mechi ya robo fainali kati ya Super Eagles na Angola siku ya Ijumaa. Lakini pia sio VO9 pekee, nyota wengine; William Troost-Ekong, Simon Moses na wengine wawili wa Cameroon wamehusishwa na kuchukuliwa vipimo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad