Mechi Kati ya Morocco na Tanzania yasubiriwa kwa hamu kwenye michuano ya Afcon






Wakati tukiendelea kufutilia mambo kwenye michuano ya Afcon, huko Ivory Coast, wapenzi wa kandanda Jumatano wanasubiri kwa hamu kuona namna mambo yatakavyokuwa kati ya Morocco na Tanzania kwenye uwanja wa San Pedro.

Timu hizo zilizopo kwenye kundi F, pia zinajipata pamoja na DRC na Zambia, ingawa matumaini makubwa ya wapernzi wa soka yapo kwenye timu ya Morocco, kutokana na historia yao ya muda mrefu, na hasa ikizingatiwa umaahiri wao kwenye kombe la dunia la 2022. Hata hivyo timu hiyo ya Atlas Lions, iliwahi kushinda kombe la AFCON, hapo 1976, licha ya kuwa na wachezaji wazuri katika kila michuano.

Jumanne Namibia imeshangaza wengi baada ya kucharaza Tunisia moja bila. Namibia sasa wanajipata kwenye nafasi ya pili kwenye orodha ya magoli ikifuata Mali ambayo ilipata 2-0 dhidi ya Afrika Kusini kwenye kundi E. Kumbuka kwamba tutaendele kukuletea habari za AFCON kadri zinavyotufikia kwenye matangazo yote yetu ya VOA.



Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad