Messi Mchezaji Bora wa FIFA 2023, Amshinda Haaland

 

Messi Mchezaji Bora wa FIFA 2023, Amshinda Haaland

Staa wa #Argentina na #InterMiami, #LionelMessi ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa FIFA 2023 kwa Wanaume akimshinda #ErlingHaaland wa Norway na #ManchesterCity aliyeshika nafasi ya pili katika Tuzo hizo zinazoandaliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (#FIFA)


Wawili hao wamelingana pointi 48 katika Mfumo wa Kura uliowahusisha Walimu na Manahodha wa Timu za Taifa pamoja na Waandishi wa Habari za Michezo lakini Messi ameshinda kwa kuwa amepata pointi 107 za kuchaguliwa kuwa “Chaguo la Kwanza” katika Mfumo wa Upigaji Kura dhidi ya 64 alizopata Haaland


Aidha, Messi ambaye ni Nahodha wa Argentina kura yake aliipeleka kwa Haaland akimchagua kuwa Mchezaji Bora wa FIFA. Washindi wengine ni #Ederson (Man. City) amekuwa Kipa Bora huku #PepGuardiola (Man. City) akitwaa Tuzo ya Kocha Bora


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad