Huduma Kwa Wanachama Wa NHIF Hazijazuiliwa




Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umesema huduma za matibabu kwa wanachama wake wote zinaendelea kutolewa katika vituo vyote vilivyosajiliwa na mfuko huo, ambavyo vipo zaidi ya 9,000, vikiwemo vya Binafsi, Madhehebu ya Dini na Serikali.
.
Mfuko huo umetoa taarifa hiyo kufuatia kusambaa kwa taarifa katika mitandao ya kijamii, zikieleza kuzuiwa kwa kadi za wanachama wake, kupata huduma, ama kupewa rufaa kwenye hospitali binafsi zilizosajiliwa na mfuko huo, taarifa ambazo umesema si za kweli na kwamba zina nia ovu ya kuleta taharuki kwa wanachama wa Mfuko huo. 
.
Aidha, Mfuko huo umesema endapo mwanachama wake atakutana na changamoto ya kukataliwa kupewa huduma katika Kituo cha huduma za afya, atoe taarifa kwenye ofisi za mfuko huo, zilizopo karibu au apige simu namba 199. 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad