Mikel Arteta Awatia Simanzi Mashabiki

Mikel Arteta Awatia Simanzi Mashabiki


Kocha Mkuu wa Arsenal amewanyong’onyesha na kuwachosha mashabiki wa timu hiyo baada ya kutoa kauli zilizoashiria timu hiyo haina mpango wa kufanya maboresho waliyotarajia katika dirisha hili.


Arteta amesema yeye na benchi lake wanawaamini wachezaji wote waliopo kikosini kwa sasa na kusisisitiza ili kushindana na timu nyingine kubwa katika kipindi hiki wanatakiwa kuwahakikishia wanawaamini.


“Tunawapenda wachezaji wetu, pia tunatakiwa kuwafanya waamini na wahisi tuna imani kubwa nao, wakiwa wanahisi hatuwaamii inaweza ikawa ngumu kuisaidia timu.”


Mzize, Maxi wakumbuka VIBE la Wananchi

Mashabiki wengi wa washika mitutu wamekuwa wakidai timu yao inahitaji Mshambuliaji mpya dirisha hili ili ifanye vizuri zaidi lakini Arteta haamini hivyo.


Kulikuwa na tetesi huenda wakamsajili mshambuliji wa Brentford, Ivan Toney lakini inadaiwa mchakato umefeli kwa sababu Arteta haonekani kumhitaji, vile vile kiasi cha pesa kinachohitajika na Brentford ni kikubwa.


Mapema mwezi huu Arteta alisema haoni kama ni suala lenye uhalisia wao kusajili Mshambuliaji katika dirisha hili.


Kocha Mashujaa FC na mpango kazi

“Kazi yangu na jukumu la benchi la ufundi kwa jumla ni kuboresha viwango vya mastaa wetu na kupata matokeo mazuri kupitia wao.”


Inadaiwa Arteta anataka kusubiri hadi mwisho wa msimu kwenye dirisha la majira ya kiangazi kwa ajili ya kufanya maboresho ya eneo lao la ushambuliaji.


Kwa sasa Arsenal inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England baada ya kucheza mechi 21 na kukusanya pointi 43.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad