Kufuatia maneno mengi ambayo yamekuwa yakizungumzwa katika mitandao ya kijamii baada ya Msanii @Harmonize_tz na Mrembo @PoshyQueeen kuweka wazi kuwa wamezama penzini, Poshy ameamua kuvunja ukimya kuhusu story za yeye kuwahi kutoka kimapenzi na @DjSevenWorldwide ambaye amewahi kuwa Official Dj wa Harmonize.
Kupitia Insta Story Poshy ameandika “I wasn’t going to talk about this, but i think at this point for the sake of me and my man’s image, with all sincerity I have never at any point in life dated seven, used to be a friend and we have worked together he knows the truth, am not that stupid, please respect my man and stop the drama”
Akimaanisha -“Sikuwahi kuzungumza juu ya hili, lakini nadhani kwa sasa kwa faida yangu na heshima ya mtu wangu katika jamii, kwa uaminifu wote sijawahi katika maisha kutoka kimapenzi na Seven, niliwahi kuwa rafiki na tumefanya kazi pamoja. anajua ukweli, mimi sio mjinga, tafadhali mwanaume wangu aheshimiwe na acheni drama”