Mwakinyo: Mpinzani Wangu Asipotokea Nitazichapa na Promota

Mwakinyo: Mpinzani Wangu Asipotokea Nitazichapa na Promota


Bondia namba moja Tanzania, amewatoa shaka mashabiki wa ngumi kuwa pambano lake litapigwa na kuahidi kuwaonyesha uwezo na kutoa burudani.


Mwakinyo anatarajia kupanda ulingoni dhidi ya Mbiya Kanku wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) katika pambano la mtata mtatuzi litakalopigwa Januari 27, 2024 katika Uwanja wa ndani wa New Amaan Visiwani Zanzibar.


Kauli hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa huenda pambano hilo lililopewa jina la 'Mtata Mtatuzi' likavunjika tena, kwani kuna baadhi ya watu wamekuwa na nia mbaya humtumia ujumbe mpinzani wake wakimtaka asipigane ili pambano hilo livunjike.


Akizungumza na Wanahabari leo Januari 25,2024 bandarini Jijini Dar es Salaam wakati akijiandaa na safari visiwa vya Karafuu (ZANZIBAR) Mwakinyo amesema amejipanga kuonesha mchezo ambao wengi hawajahi kuuona huku, akiahidi kutoa burudani kwa mashabiki wake.


“Mpaka sasa kila kitu kipo katika ubora kuelekea pambano langu. Lakini kuna changamoto kidogo kwa upande wa promota na kwangu pia inani confuse lakini sioni kama ni taarifa mbaya kwangu kwa sababu mashabiki zangu wana hamu wanione nikipigana, kwa hiyo mwisho wa siku lazima nipigane.


“Kuna maneno ya kwamba wapo baadhi ya watu wanamtumia meseji mpinzani wangu ili asitokee kwenye pambano ili liahirishwe na nionekane kwamba ni kawaida yangu kuharibu mapambano.


“Lakini ambacho tumekubaliana na promota (Meja Selemani Semunyu) ni kwamba iwapo kitatokea kitu kama hicho basi tutacheza mimi na yeye ilimradi mashabiki zangu wafurahi.


“Wengi wanaotamani wanione nikipigana ni wale wapenda maendeleo na wapenda ngumi, lakini kuna vikundi vya watu wachache wapinga maendeleo wenye roho mbaya nadhani ndiyo wanataka hivyo. Wanawaza nguvu yangu itakuwa wapi baada ya mimi kushinda pambano hilo, ndiyo maana wanakosa usingizi.


“Mimi ni kijana ninayepambania ndoto zangu, nimejiandaa vizuri ndani ya pambano nan je ya pambano, niko vizuri kote kote, kila kitakachotokea nimejiandaa kukabiliana nacho,” amesema Mwakinyo.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad