Mwanajeshi Aliyeua Mke na Mama Mkwe Kisha naye Kuuawa, Kuzikwa kesho

Mwanajeshi aliyeua mke na mama mkwe kisha naye kuuawa, kuzikwa kesho


Miili ya watu watatu wakazi wa Mtaa wa Segu Chini Kata ya Nala mkoani Dodoma waliofariki Jumapili ya Januari 29 mwaka huu, inatarajiwa kuzikwa Jumanne na Jumatano wiki hii mara baada ya taratibu za mazishi kukamilika.


Marehemu hao ni Festo Maganga ambaye ni mwanajeshi mstaafu aliyedaiwa kumuua mke wake pamoja na mama mkwe wake, huku chanzo kikidaiwa ni ugomvi wa mara kwa mara kati yao uliokuwa ukisababishwa na wivu wa mapenzi.


Emmanuel Chugulu ambaye ni jirani wa marehemu amesema siku ya tukio majira ya saa tisa akiwa machungoni alipokea simu akijulishwa tukio hilo.


Akiwa njiani kurudi alikutana na marehemu Maganga akiwa katika hali ya kuchanganyikiwa na kumwambia kuwa ameua mkewe na mama mkwe kwa sababu wamekuwa wakimtukana mara kwa mara.


Baaada ya kutoa maelezo hayo, Maganga aliomba msaada wa kupelekwa kwa mwenyekiti. Chugulu amedai kuwa muda mfupi baadaye alipata taarifa za kuuawa kwa Maganga baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira.


Viongozi wa serikali ya mtaa wamewashauri wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi.


Jitihada za kumpata kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma kuzungumzia tukio hilo zimeshindikana baada ya kuwa nje ya ofisi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad