Mzee wa Kanisa Akutwa Amefariki Gesti Akiwa na mwanamke

 

Mzee wa Kanisa Akutwa Amefariki Gesti Akiwa na mwanamke

Uchunguzi unaendelea baada ya mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 60 kupatikana amefariki ndani ya nyumba ya kulala wageni katika eneo la Kapsoit, kaunti ndogo ya Belgut, kaunti ya Kericho.


Mwili wa David Kiplangat Ronoh ambaye anasemekana kuwa mzee wa kanisa moja la eneo hilo uligunduliwa siku ya Jumatano usiku katika moja ya vyumba vya kulala wageni vya Simbi Bar and Lodge.


Uchunguzi wa awali umebaini kuwa marehemu alikuwa ameandamana na mwanamke asiyetambulishwa wakati alipopanga chumba hicho siku ya Jumatano jioni. Mwanadada huyo anaripotiwa kuchukua hatua ya kuripoti tukio hilo la kushangaza kabla ya kutoweka asipatikane tena.


Huku akithibitisha kisa hicho, mkuu wa polisi katika kaunti ndogo ya Belgut, Bw Charles Kibati alisema kuwa mwili wa marehemu haukuonyesha majeraha yoyote. Kondomu iliyotumika hata hivyo ilipatikana kando ya mwili wa marehemu.


Mwili wa mzee huyo wa kanisa ulipelekwa katika hifadhi ya maiti ya Hospitali ya Rufaa ya kaunti ya Kericho kwa uchunguzi wa mauti huku polisi wakiendelea na msako wa mwanadad ambaye alikuwa ameandamana naye ili kusaidia katika uchunguzi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad