Ndege zagongana Japan, watano wafariki dunia




Japan. Watu watano waliokuwa kwenye ndege ya walinzi wa Pwani ya Japan wamefariki dunia baada ya ndege yao kugongana na ndege ya abiria katika uwanja wa ndege wa Haneda jijini Tokyo.

Kwa mujibu wa tovuti ya BBC, Ndege hiyo ilikuwa ikipeleka msaada katika maeneo yaliyokumbwa na tetemeko kuu la ardhi la Januari 1, 2024.

Watu wote 379 waliokuwa kwenye ndege ya abiria inayomilikiwa na shirika la ndege la Japan Airways iliyowaka moto katika ajali hiyo, waliokolewa.

Picha za video zilionyesha abiria wakitoka katika mlango maalumu wa dharula wa ndege katika harakati za kujaribu kuokoa uhai wao.

Kufuatia tukio hilo, Waziri Mkuu wa Japan, Fumio Kishida amezungumza na waandishi wa habari na kuthibitisha wafanyakazi watano kati ya sita kwenye ndege ya walinzi wa pwani walifariki dunia wakati wakiendelea na shughuli ya kupeleka msaada kwa watu walioathirika na tetemeko la ardhi la jana Jumatatu.

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa kipimo cha richa 7.6 lilipiga Japan siku ya mwaka mpya saa 4:10 asubuhi saa za ndani wakati watu wengi walikuwa wakitembelea familia na kusherehekea na kusababisha vifo na uharibifu mkubwa wa majengo na miundombinu.

Imeandaliwa na Victor Tullo kwa msaada wa mashirika.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad