Paul Makonda "Kwenye Mdahalo Mje Watatu Mimi Nitakuwa Peke Yangu"


Wito wangu kwa Kaka yangu Mbowe kabla haujaenda barabarani , sisi hatusemi kwamba usiende, zipo Mamlaka zinazohusu utaratibu namna gani uweze kuandamana, kwasababu Rais wetu anasimamia four R na anazingatia ujenzi wa demokrasia na yeye msingi wake ni maridhiano”

“Nakuomba Kaka yangu Mbowe, wewe pamoja na Ndugu yangu Mnyika na Kaka yangu Lissu kabla hamjawapeleka Watanzania barabarani Mimi kama Mwenezi wa CCM, nipo tayari tufanye mdahalo wa wazi na mdahalo huu ningetamani uandaliwe na Wanahabari na ikikupendeza Kaka yangu Mbowe uchague Wanahabari unaowataka watakaondaa mdahalo huu,

“Wewe Mbowe uje na Timu yako Mimi nitakuja pekee yangu sina sababu ya kukisumbua Chama kubeba Watu wengi, pale tupate nafasi ya kuwaeleza yale ambayo wewe unayasema ya kuwapeleka Watanzania barabarani na Mimi nitakayosema ili Watanzania wachaguw wanaenda barabarani kwenda kuvuruga uchumi wa Taifa lao au wanabaki kujenga maridhiano na umoja wa Kitaifa chini ya Dkt. Samia Mwenyekiti wetu wa CCM” — Paul Makonda ( @baba_keagan ) Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad