Polisi Wawakana Chadema Mchana Kweupe "Bado Hatujaafikiana nao Kuhusu Kuwaruhusu Kuandamana"

Polisi Wawakana Chadema Mchana Kweupe "Hatujaafikiana nao Kuhusu Kuwaruhusu Kuandamana"


DEMOKRASIA: Baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kuandika kwenye Ukurasa wake kwenye Mtandao wa X, kuwa wamekubaliana na Jeshi la Polisi kuwa #Maandamano ya Januari 24, 2024 yataendelea kama ilivyopangwa, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro amesema hawajakubali au kukataa maandamano yao na wamekubaliana watawapa majibu yao kimaandishi kesho Januari 23, 2024

Amesema “Hatujaawambia maandamano yapo au hayapo, kwasababu walituandikia barua kwenye Himaya zao na sisi majibu watayapata kwenye Himaya walizoandika barua hizo, ambapo utakuwa ndio mwongozo wa nini kinafanyika huku tukizingatia masuala ya kiusalama na Maslahi ya Taifa kwa ujumla. Tumezingatia suala la Amani na majibu yao watayapata kesho”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad