Rais Dr Hussein Mwinyi Apangua Baraza la Mawaziri Zanzibar


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amefanya mabadiliko ya Baraza la Mapinduzi kwa kuteua mawaziri wapya wawili na kumbadilisha wizara waziri mmoja.

Rais pia ameteua Naibu Mawaziri wapya wawili na kumbadilisha wizara Naibu Waziri mmoja. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Taarifa iliyoyolewa leo Jumamosi Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena Said na uteuzi wa viongozi hao umeanza leo.

Katika taarifa hiyo ametaja viongozi hao walioteuliwa kuwa ni Mudrik Ramadhan Soraga ameteuliwa kuwa Waziri wa Utali na Mambo ya Kale.

Kabla ya Uteuzi Mudrik alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji.

Ikumbukwe kuwa Mudrik ameteuliwa siku moja baada ya Simai Mohamed Said kutangaza kujiuzulu wadhifa wake wa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Serikali hiyo.

Ali Suleiman Ameir (Mrembo) ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Ikulu. Kabla ya Uteuzi Ali alikuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango.

Shaaban Ali Othman ameteuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi. Kabla ya Uteuzi Mheshimiwa Shaaban alikuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini.


Juma Makungu Juma ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango. Kabla ya Uteuzi Juma alikuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi.

Salha Mohamed Mwinjuma ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi. Salha ni Mwakilishi wa Viti Maalum kutaka Kundi la Vijana Kusini, Unguja.

Zawadi Amour Nassor ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini. Zawadi ni Mwakilishi wa Jimbo la Konde, Mkoa wa Kaskazini, Pemba.

Aidha, amesema viongozi walioteuliwa wataapishwa katika tarehe ambayo itatangazwa baadae.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad