Rais Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi milioni 150 kuchangia ujenzi wa Kanisa la KKKT la Bethel Usharika wa Nshara Machame Mkoani Kilimanjaro anakosali Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe.
Akizungumza leo katika ibada ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi huo, Mwenyekiti Freeman Mbowe ambaye husali katika Kanisa hilo awapo nyumbani Machame amesema alishirikisha watu mbalimbali kuhusu kuchangia ambapo miongoni mwao ni Rais Samia.