Rais Samia Azichangia Timu za Taifa Milioni 500


Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amezichangia Timu za Taifa Tsh. milioni 500 kupitia harambee ya kuchangia Timu hizo iliyofanyika Jijini Dar es salaam usiku huu ikiongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Kamati ya Hamasa.

Akiongea na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa njia ya simu, Rais Samia amenukuliwa akisema “Michezo ni jukumu letu, ni jukumu la Serikali ni jukumu la Watanzania, Serikali kama mnavyojua tumejitahidi sana kukuza michezo”

“Michezo ni pia ni gharama Ndugu zangu, Serikali tumejitahidi tumetoa vivutio, Timu zimetuitikia lakini imefika mahali tuna uchache wa bajeti, kwahiyo niwaombe tuchange ili Timu zetu wakacheze kwa moyo na waende wakashindane na sio kushiriki”

“Kwa kuanzia nimezunguka huku na huku, Mimi Mkuu wa Nchi na Marafiki zangu wameniahidi na wamesema tutachangia Tsh.milioni 500 hiyo ndio kitangulizi na kifungua michango”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad