Rais Samia: Suala la Bima ya Afya Haliepukiki

 

Rais Samia: Suala la Bima ya Afya Haliepukiki

Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema ili kuendelea kutoa huduma za afya endelevu suala la bima ya afya kwa kila mtu haliepukiki.


Amebainisha hayo wakati wa ufunguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lumumba na kusema hospitali hiyo itasaidia kupunguza msongamano wa wagonjwa na kutoa huduma bora zinazokusudiwa.


"Suala la bima ya afya haliepukiki tujipange kila mmoja kuwa na bima ili tutibiwe vile ipasavyo,” amesisitiza Rais Samia.


Pia ameeleza kufarijika kuwepo kwa wataalamu katika hospitali hiyo, na kutoa rai kwa Wizara ya Afya kuhakikisha inaendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad