Roma: Freshi tu Chid kanifunika kwenye ngoma yangu!



Mijadala ilikuwa mingi baada ya kuachiwa kwa wimbo wa ‘Naskia Harufu’ ya kwake Roma ft Chid Benz ambapo kila mmoja akija na mtazamo wake binafsi kuhusu project hiyo japo wengi wakidai kuwa Chid kamkalisha Roma humo ndani!


Roma amekutana na comments hizo lakini kwa mujibu wake, anaona fresh tu lakini kinachomchanganya ni pale ambapo hao wanaotoa comments hizo ndio hao hao wanazitumia punch lines zake kutoka kwenye verses zake za wimbo huo na kuzitumia katika mitandao yao ya kijamii!


"Fresh tu mi naona sawa tu Chid akinifunika maana ni kweli mimi nimeandika vizuri lakini si unajua lisauti la Chid zito," alisema Roma.


Alieleza hayo kupitia kipindi cha Clouds FM Top20.


Mtazamo wako umesimama vipi ni nani kamkalisha mwenzake humo ndani kati ya Roma na Chidi na unadhani ni kwa vigezo vipi!?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad