TETESI: Benchikha Amkataa Clatous Chama




Inasemekana Viongozi wa klabu ya Simba watakuwa na kikao cha nidhamu na kiungo wao Raia wa Zambia Clatous Chama leo kwa njia ya mtandao akiwa huko huko Zambia kwenye majukumu ya Timu ya Taifa.

Kocha wa kikosi cha wekundu wa Msimbazi Abdelhak Benchikha hajafurahishwa na nidhamu ya Chama hata baada ya kumkosea kocha wa Viungo hakujaribu kuomba hata radhi na akionekana akitoa vijembe kwenye mitandao ya kijamii, hatua hiyo imemfanya Benchikha kawaambia mabosi wa Simba kuwa anahitaji mbadala wa Chama atakayeweza kuziba nafasi yake vyema, Benchikha alisema hataki mchezaji ambaye atajiona yupo juu ya makocha, wachezaji na hata Viongozi.

Huu huenda ukawa mwisho wa mwamba wa Lusaka katika kikosi cha Msimbazi, Je mashabiki watakubaliana na kuachwa kwa mchezaji wao pendwa Chama!?

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad