TIMU Simba Watambulisha Mshambuliaji mpya

TIMU Simba Watambulisha Mshambuliaji mpya


Klabu ya Simba imethibitisha kukamilisha usajili wa Mshambuliaji raia wa Gambia Pa Omar Jobe (25) kwa Mkataba wa miaka miwili.

Simba imemtambulisha mshambuliaji wake mpya, Pa Omar Jobe ambaye kwenye picha zake za huko alikokuwa akicheza anaonekana kupendelea kuvaa jezi namba tisa ambayo imekuwa ikigomewa na mastaa wengi ndani ya kikosi cha Wekundu wa Msimbazi ikitafsiriwa kwamba ina gundu klabuni hapo.


Mara ya mwisho jezi namba tisa ndani ya kikosi cha Simba ilivaliwa na mshambuliaji raia wa Burundi, Laudit Mavugo ambaye hakufanya vizuri ndani ya kikosi cha Simba na baadaye kupewa mkono wa kwaheri.


Mshambuliaji huyo mpya wa Simba kutoka klabu ya FC Zhenis Astana ya Ligi Kuu ya Kazakhstan, Jobe atafuata nyayo za mastaa waliopita hivi karibuni na kuikataa jezi hiyo au atavaa kama ilivyokuwa kwa mastaa hawa?


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad