TMA Yatoa Tahadhari Mvua Kubwa Mikoa Nane

TMA Yatoa Tahadhari Mvua Kubwa Mikoa Nane

TMA Yatoa Tahadhari Mvua Kubwa Mikoa Nane


Dar es Salaam. Kama unaishi mikoa ya Morogoro, Lindi, Iringa, Mtwara, Mbeya, Songwe, Njombe na Ruvuma, basi kaa mguu sawa kwani Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo kuhusu uwepo wa hali mbaya ya hewa kwa siku tano.

Utabiri huo unakuja siku chache tangu baadhi ya mikoa kama Dar es Salaam na Morogoro kushuhudia mvua kubwa iliyoathiri miundombinu na kusababisha vifo.

Utabiri huo wa TMA uliotolewa leo Januari 29,2024 utaanza kesho Januari 30 na utadumu hadi Februari 2 mwaka huu.

“Angalizo la mvua kubwa limetolewa katika maeneo machache ya mikoa ya Morogoro, Lindi, Mtwara, Iringa, Mbeya, Songwe, Njombe na Ruvuma,”imeandikwa kwenye taarifa hiyo.

Wakazi katika mikoa hiyo watashuhudia athari ya makazi yao kuzungukwa na maji, pamoja na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi.

Mkoani Morogoro hivi karibuni waliripotiwa watu watano kufariki dunia na wengine 246 kuokolewa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha mjini Morogoro na kusababisha mafuriko yaliyoharibu makazi na barabara.

Kwa Mkoa wa Dar es Salaam mvua hizo zilisababisha barabara kutopitika, nyumba kuzingirwa maji na wananchi kupita  adha ya usafiri.

Mara kadhaa Serikali imekuwa ikisisitiza wananchi wote waliojenga bondeni kuhama mara moja kuepuka athari za mvua.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad