TRA yavunja rekodi yakusanya trilioni hizi.

 

TRA yavunja rekodi yakusanya trilioni hizi.

Menejimenti ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi imesema leo kuwa katika kipindi cha mwezi December 2023 pekee, TRA imefanikiwa kuvunja rekodi mpya ya kukusanya kiwango kikubwa cha makusanyo ndani ya mwezi mmoja (December 2023) ikiwa ni mara ya kwanza kukusanya kiwango kikubwa toka kuanzishwa kwa TRA.


Taarifa mpya ya TRA leo imeeleza kuwa kiasi kilichokusanywa kwa mwezi December 2023 pekee ni Tsh. trilioni tatu nukta sifuri tano ( Trilioni 3.05) ikiwa ni ufanisi wa asilimia mia moja na mbili nukta tisatisa ambapo lengo lilikuwa ni kukusanya Tsh. trilioni 2.96.


TRA ambayo inaongozwa na Kamishna Mkuu Alphayo J. Kidata imesema makusanyo haya ni ongezeko la 9.2% ukilinganisha na kiasi cha Tsh. trilioni 2.79 kilichokusanywa katika mwezi kama huu katika mwaka wa fedha 2022/23.


Taarifa zaidi kuhusu makusanyo ya kodi ya nusu ya mwaka wa fedha 2023/2024 kukujia.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad