Sakata linaloendela la Harmonize na DJ wake @djsevenworldwide kuwa ugomvi wao umetokana na Harmonize kumchukua mwanamke wa DJ wake halijaanzia kwa Posh Queen pekee.
Baada ya Harmonize kuvunja mahusiano yake na Kajala yale ya mwanzo kabla ya kurudiana mara ya pili Harmonize alikuja kutoka Marekani na mwanamke aliyejulikana kwa jina la Brian.
Baada ya kutua Tanzania DJ seven aliwahi kupost video zikionyesha akiwa na Brian kabla ya kuwa an Harmonize na wengi walipuuzia wakihisi DJ Seven anatafuta kiki kupitia mwanamke wa Boss wake.
Hii video inaonyesha mwanzoni DJ Seven akiwa na Posh Queen wakifanya kazi ya U’DJ na mwishoni inaonyesha akiwa na Brian kabla ya kuchukuliwa na Harmonize.
Kwa taarifa kutoka kwa mtu wa karibu wa Harmonize na DJ Seven ameiambia Bongo5 kuwa Ukweli ni kwama hata Brian alikuwa mwanamke wa DJ Seven kabla ya Harmonize kumchukua.
Mtu huyo anasema kuwa Mara hii DJ Seven ameshindwa kuivumilia tabia ya boss wake ya kuchukua wanawake wake, DJ Seven ameichukua kama Harmonize anatumia fimo ya pesa kuchukua wanawake zake na ndio maana mara hii ameamua kuondoka na kuacha kufanya naye kazi kabisa ili kuepusha mengine.
Kama mnakumbuka DJ Seven aliwahi kuandika maneno mengi akisema mara nyingi marafiki ndio watu wabaya, mnaongea mnacheka kumbe anakuzunguka kwa mwanamke wako.
Kauli hiyo DJ Seven alikuwa anamlenga Boss wake Harmonize.
Siku kadhaa nyuma Harmonize ameonekana akiwa na Posh Queen Mbugani wakitalii wote na jana Posh Queen amempost Harmonize jambo ambalo linamaanisha Posh Queen ameamua kuweka wazi mahusiano yake na Harmonize.
Leo Harmonize amethibitisha kwamba hawapo sawa na aliyekuwa DJ wake kisa kudaiwa kumchukua mwanamke wake na amesema hata kama ana tamaa kiasi gani hawezi ku’share na ndugu.
Unahisi kwanini Harmonize amemfanyia hivi DJ wake?? Jambo hili lingekutokea wewe ungechukua hatua gani??