Usajili Dirisha Dogo: Simba, Yanga, Azam Moto unawaka

 

Usajili Dirisha Dogo: Simba, Yanga, Azam Moto unawaka



Vita ya usajili wa dirisha dogo kwenye Ligi Kuu Bara imezidi kupamba moto ambapo timu mbalimbali zimeendelea kufanya maboresho kwa kushusha mashine za maana kwa ajili ya kuhakikisha wanakuwa na vikosi imara vya kushindania ubingwa.


Kwa upande wa tatu bora ya timu ambazo zinapewa nafasi kubwa ya kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu kutokana na kasi yao, yaani Azam, Yanga na Simba, tayari kila timu imeonesha makucha kwa kutangaza majembe mapya kwenye dirisha hili dogo lililofungwa Desemba 16, 2023 ambapo upande huu ukiweka kigingi, mwingine anaweka chuma.


Yanga ndiyo ilikuwa timu ya kwanza ambapo mara tu, baada ya kukamilisha usajili wa kiungo fundi kutoka JKU ya Zanzibar, Shekhan Ibrahim, walimtangaza rasmi kwenye mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar uliopigwa Desemba 16, 2023.


Baada ya hapo ikawa zamu ya Azam kuiteka shoo ambapo walitambulisha majembe mawili kwa mpigo wakianza na straika Mcolombia, Franklin Navarro, Desemba 28, 2023, kabla ya kumtambulisha kipa Msudani, Mohamed Mustafa, Desemba 31, 2023.


Usiku wa kuamkia mwaka huu wa 2024, Yanga wakaibuka tena na kumtangaza nyota wa zamani wa Simba, Augustine Okrah tukio lililofanyika kwenye mchezo dhidi ya JKU.


Simba ambao wanakamatia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, nao baada ya kuwa kimya muda mrefu, jana Jumatatu wakafungua pazia la utambulisho wa dirisha dogo kwa kumtangaza rasmi, Saleh Karabaka kutoka JKU ya Zanzibar kwa mkataba wa miaka mitatu.


Ikumbukwe dirisha dogo la usajili bado lipo wazi hadi Januari 15, 2024 na Spoti Xtra, linajua bado kuna listi kubwa ya wachezaji ambao wako mbioni kutangazwa ndani ya Simba, Yanga na Azam.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad