Wachezaji Watatu Waliotemwa Simba Wapata Dili Pengine Fasta

 

Wachezaji Watatu Waliotemwa Simba Wapata Dili Pengine

Nyota watatu kati ya sita waliotemwa na Simba katika dirisha dogo, Nassor Kapama, Jimmyson Mwanuke na Shaaban Idd Chilunda wamepata dili baada ya kunaswa na Mtibwa Sugar na KMC.


Mwanuke na Kapama wametua zao Mtibwa, wakati Chilunda aliyewahi kuwika na Azam FC akisajiliwa KMC ili kuendeleza moto alioshindwa kuuwasha Msimbazi.


Akizungumza na Mwanaspoti, Kapama alisema ni kweli amemalizana na Mtibwa kwa mkataba wa miezi sita baada ya kuvunjiwa mkataba na Simba sasa atakuwa huko kuipambania timu hiyo isishuke daraja.


“Nimemalizana na Mtibwa nitacheza huko kwa miezi sita naamini ni chaguo sahihi baada ya ofa nyingi nilizokuwa nazo naamini nitapambana kwa kushirikiana na wenzangu ili kuiondoa timu hiyo kwenye hatari ya kushuka daraja.” alisema Kapana.


Wakati huohuo rafiki wa karibu wa Mwanuke ameliambia gazeti hili kuwa beki huyo amejiunga na Mtibwa kwa mkopo akitokea Simba.


“Mwanuke ametolewa kwa mkopo na Simba ili aweze kuisaidia Mtibwa kukwepa janga la kushuka daraja kutokana na kuwa katika nafasi mbaya,” kilisema chanzo.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad