Wafanyakazi wa SGR, Dar, Singida na Tabora Wagoma Wakishinikiza Walipwe Mishahara
Baadhi ya Wafanyakazi wanaoshiriki katika Ujenzi wa Mradi wa Reli ya Kisasa ya #SGR katika Kambi ya Tabora, Itigi (Singida), Dodoma na Ilala (Dar es Salaam) wamegoma kufanya kazi leo Jumamosi Januari 6, 2024 wakishinikiza kulipwa mshahara wa Desemba 2023 kutoka kwa Mkandarasi Mkuu wa Mradi, Kampuni ya #YapiMerkezi
Imedaiwa Wafanyakazi hao wamefikia hatua ya kugoma kutokana na Mkandarasi kutotoa taarifa yoyote juu ya malipo yao kila wanapouliza, ikumbukwe kuwa hivi karibuni Yapi ilitangaza kupunguza zaidi ya Wafanyakazi 600 kutokana na sababu mbalimbali