Wanajeshi, Polisi na FFU Kufanya Usafi Dar es Salaam Januari 23-24

 

Wanajeshi, Polisi na FFU Kufanya Usafi Dar es Salaam Januari 23-24

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila ametangaza kufanyika kwa zoezi la usafi katika Wilaya zote 5 kuanzia January 23 hadi 24 January zoezi ambalo litahusisha Wanajeshi zaidi ya 5000, Polisi zaidi ya 3000, FFU na Vyombo vingine vya dola.


RC Chalamila ameyasema hayo leo katika ibada ya kuwekwa Wakfu Mwangalizi wa Jimbo la Babtist la Dar es Salaam, Makamu , Katibu, Katibu Msaidizi, Mhasibu na Mhasibu Msaidizi ambapo amewataka Wakazi wa Dar es Salaam kutokuwa na shaka watakapoviona Vyombo vya Dola vikifanya usafi.


Chalamila amesema katika kufanya usafi huo pia kutakuwa na magari mbalimbali ya kijeshi kwa ajili ya kukusanya takataka na kuwataka Waumini kuwa Mabalozi wazuri wa kampeni ya usafi ili kupambana na magonjwa mbalimbali.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad