Washambuliaji Simba Wamtesa Benchikha

 


Kocha wa Simba, Abdelhak Benchikha amebakiza maeneo machache kuboresha kikosi, lakini kubwa ni lile la ushambuliaji.


Benchikha ameliambia Mwanaspoti kwamba, anafurahia maboresho na wachezaji wanavyoendelea kuimarika, ila bado hajaridhishwa na idadi ya matumizi ya nafasi ambazo wanatengeneza uwanjani.


Kocha huyo alisema kikosi hicho kinazuia vizuri mashambulizi licha ya mabadiliko machache ya eneo la ulinzi, lakini lile la kiungo linafanya kazi nzuri isipokuwa changamoto ipo mwisho.


Alisema anatamani washambuliaji waongeze umakini wa kutumia nafasi ikiwemo shabaha ili kikosi kishinde kwa idadi kubwa ya mabao kama ambavyo kinavyotengeneza nafasi.


Katika mechi nne za Mapinduzi, Simba imefunga mabao tisa ambapo dozi ya ushindi mkubwa ni mabao matatu ilioupata kwenye michezo mbili tofauti huku ikiruhusu mabao mawili.


Idadi hiyo ni ndogo kulinganisha na nafasi nyingi ambazo imekuwa ikizitengeneza kwenye mechi ambapo eneo linalokwamisha ni utulivu wa washambuliaji kuzitumia. “Tunahitaji kuongeza utulivu sio ushindi ambao tunatakiwa kuufurahia wakati tunatengeneza nafasi nyingi za kufunga. Tunahitaji kuendelea kuimarisha hili eneo la mwisho,” alisema Benchikha.


“Kuna wakati ukiangalia nafasi ambazo tunapoteza unapata hudhuni na hasira, lakini ni kazi yetu kuendelea kuwapa maelekezo wachezaji kama wanaweza kuimarika au tuangalie namna nyingine.”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad