Watu 22 wafariki dunia Simiyu kwa kufunikwa na gema mgodini



Simiyu. Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu wamefariki dunia baada ya kufunikwa na gema katika mgodi wa Ikinabushu Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 14, 2024, baada ya kazi ya siku mbili ya uokozi iliyoanza mara baada ya ajali hiyo iliyotokea Saa 11:00 alfajiri ya kuamkia Januari 13, 2024, Kaimu Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Simiyu, Faustine Mtitu amesema na kuwa miili ya watu hao imeopolewa.

"Baada ya kazi ya siku mbili mfululizo ya uokozi, kikosi cha uokoaji kinachojumuisha wananchi, askari na wataalamu kutoka vikosi na taasisi mbalimbali za Serikal, kimefanikiwa kuopoa miili ya watu wote waliofunikwa na ngema na tumejiridhisha kuwa hakuna miili iliyosalia ndani ya mgodi," amesema Kamanda Mtitu

Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Bodi ya Mgodi wa dhahabu Ikinabushu, Masumbuko Jumanne amesema waliopoteza maisha katika ajali hiyo waliingia mgodini kwa kujipenyeza kinyume cha taratibu kutokana shughuli za uchimbaji kusitishwa.

"Maafa haya yametokea wakati uongozi umesitisha shughuli za uchimbaji kutoa fursa ya kutekeleza maagizo na maelekezo kuhusu masuala ya uchimbaji salama kutoka kwa wakaguzi wa migodi waliotutembelea siku moja kabla ya ajali," amesema Masumbuko.

Amesema kabla ya ajali hiyi, uongozi wa mgodi huo kwa kushirikiana na vikosi vya ulinzi na usalama uliwaondoa watu wengine walioingia mgodini kwa kujipenyesha kinyemela nyakati za usiku.

"Wakati uongozi ukishughulikia tatizo la wale walioondolewa mgodini, huku nyuma kundi lingine la wachimbaji lilijipenyeza na kuingia mgodini baada ya kuwazidi ujanja walinzi, na matokeo yake ndio haya maafa," amesema Masumbuko.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk Yahaya Nawanda ametangaza kusitisha shughuli za uchimbaji katika migodi hiyo hadi taratibu za uchimbaji salama zitakapozingatiwa.

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde akiongozana na RC Nawanda, viongozi na watendaji kadhaa wa Serikali wamewasili Kijiji cha Ikinabushu yaliko machimbo hayo na wanaendelea na vikao vya tathmini kabla ya kutoa tamko na maagizo ya Serikali.

Mwananchi 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad