Waziri January Makamba Aingilia Kati Sakata la Kenya Airways na Air Tanzania Kuzuia

Waziri January Makamba Aingilia Kati Sakata la Kenya Airways na Air Tanzania Kuzuia


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba @jmakamba amesema amefanya mazungumzo na Waziri mwenzake anayeshughulikia masuala ya kigeni Nchini Kenya, Musalia Mudavadi na wamekubaliana kumaliza sakata linaloendelea ikiwemo zuio la Ndege za Kenya Airways kutua Tanzania.


Makamba amesema kwa Mamlaka waliyonayo wamekubaliana kumaliza jambo hilo ndani ya siku tatu .


Kauli ya Makamba inakuja saa chache baada ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), kusitisha vibali vya Shirika la Ndege la Kenya (KQ) vya kuendesha safari za ndege za abiria kati ya Nairobi na Dar es salaam chini ya vifungu vya Haki za Uhuru wa Trafiki namba tatu na nne kuanzia January 22, 2024.


Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari amesema tamko hilo limetolewa ikiwa ni njia ya kujibu mapigo kufuatia uamuzi wa Mamlaka ya Anga ya Jamhuri ya Kenya kukataa ombi la Tanzania la Kenya kusafirisha mizigo yao yote kwa kutumia Kampuni ya Air Tanzania kwa kuzingatia Haki za Trafiki nambari tano kati ya Nairobi na Nchi za dunia ya tatu kinyume na kifungu cha 4 cha Mkataba wa Makubaliano ya Huduma za Ndege, kati ya Tanzania na Kenya ambao ulitiwa saini November 24, 2016 Jijini Nairobi, Kenya.


Kwa upande wake Waziri Mudavadi ameaema “Jioni hii nimezungumza na Mh. Makamba ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuhusu uamuzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania kufuta idhini ya Shirika la Ndege la Kenya kuendesha safari za abiria kati ya Nairobi na Dar es Salaam kuanzia tarehe 22 Januari 2024, tumekubaliana kwa pamoja kwamba Mamlaka zetu za Usafiri wa Anga zitafanya kazi pamoja ili kutatua suala hili kwa amani ndani ya siku tatu zijazo, kwahiyo kusiwe na sababu za kuwa na hofu”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad