Waziri Mchengerwa Amsimamisha Kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga

 

Waziri Mchengerwa Amsimamisha Kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga Isaya Mugishangwe Menje kuanzia leo January 21,2024 ili kupisha uchunguzi.


Mchengerwa amechukua hatua hiyo baada ya kupokea taarifa za Mkurugenzi huyo kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kupelekea kulegalega kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo.


Kutokana na tuhuma hizo Mchengerwa amemuagiza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Adolf Ndunguru kutuma timu ya uchunguzi mara moja katika Halmashauri hiyo.


Hatua hii inakuja siku moja baada ya Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo (CCM) Paul Makonda akiwa ziarani Wilaya ya Pangani, Tanga kumuagiza Mkurugenzi huyo hadi kufikia kesho Jumatatu awe amemlipa Mfanyabiashara Mlemavu anayeidai Halmashauri hiyo shilingi milioni 61.5 na asipofanya hivyo ataondoka sio kwa kuhamishiwa sehemu nyingine bali kurudi nyumbani kwao ambapo Makonda alinukuliwa akisema “Jumatatu tutaangalia kama una haki yako, tutaangalia kati ya Mwenezi wa Chama na Mkurugenzi asipokulipa anaondoka sio kwenda kuhamishwa anarudi nyumbani kwao, hawa ndio wanatuchonganisha, Watu wanaichukia CCM wanamchukia Dkt. Samia kumbe kwa majibu ya hovyo tu”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad