Katika siku za hivi karibuni tangu habari za kifo cha utata cha dadake Pasta Kanyari mikononi mwa mwanamume tapeli, msanii Willy Paul amekuwa akitoa wosia kuntu kwa wasichana, haswa wale wanaopenda vya bwerere na tafrija za usiku mjini.
Msanii huyo kwa mara nyingine amerudi na ushauri wa aina hiyo, ila sasa amegusia suala nyeti kabisa kuhusu mtu Fulani maarufu mwanamume ambaye amekuwa akiwavizia wasichana kwenye tafrija.
Pozee jap hakumtaja mtu huyo, alisema kwamba anajulikana na aghalabu mawindo yake ni wasichana wa kati ya miaka 19 hadi 25 ambao baada ya kuwatia kwenye mtego wake, huwaambukiza virusi vya nduli ya UKIMWI.
“Wewe ni mtu maarufu na uko na UKIMWI, umekuwa ukiwalenga wasichana wa kati ya umri wa miaka 19 hadi 25. Umewaambukiza wasichana wasio na hatia, wengine hata hawana habari,” Willy Paul alisema.
Cha kushangaza, Willy Paul alidai kuwa msichana wa hivi punde mtu huyo aliambukiza ni ‘dadake’ na kumtaka kukoma tabia hiyo kabla hajatumbuliwa.
Willy Paul pia aliwashauri wasichana wanaohadaiwa kwa vitu ghali pasi na kuvifanyia kazi, akiwataka kujitahadhari na pia wengine kuchukua vipimo vya afya zao kama kwa njia moja au nyingine wamewahi kutana na mwanamume huyo ambaye alimuelezea pasi na kumtaja jina.
“Wa mwisho uliambukiza ni dada. Unafaa kuwa gerezani bosi, unajijua mwenyewe. Na nyinyi wasichana wa klabu na fomu za tafrjia shauri yenu. Nendeni mkapimwe, na kwa wale wenye bahati, achene tamaa,” Willy Paul alishauri.