Miongoni mwa wachezaji wa Yanga ambao hawapo kwenye majukumu ya timu za taifa ni pamoja na Pacome, Abubakar Salum, Khalid Aucho, na Yao Attoula. Hawa wote hawajaitwa kwenye timu za taifa. Ajabu ni kwamba, wachezaji hawa aidha wapo Daressalaam, au wapo Zanzibar wakizurura tu mitaani.
Na hii imekuwa tendency ya hizi timu kubwa mbili (Simba na Yanga) kwenye michuano hii ya Mapinduzi Cup. Angalau msimu huu Simba wamepeleka wachezaji wao wote ambao hawana majukumu ya National Team. Saidoo, Baleke, Onana, Kanoute, Che Malone, Ngoma, Miquisson, Ayoub, Kapombe, na Phiri wote wapo Zanzibar na wanacheza.
Ukiwa na Yanga yenye Gift Fred na Khamis Naanguka kama mabeki wa kati ambao kiuhalisia bado wachanga, sio senior player, ni rahisi sana kuzidiwa katika mchezo na kuruhusu magoli, hivyo walipaswa kuwa na wachezaji wao wenye uwezo wa kuamua matokeo kama Pacome, Max, au hata Aucho na Sure Boy ambao wapo tu hawana majukumu yoyote.
Huwezi kuwafunga APR (mabingwa wa ligi ya Rwanda msimu uliopita, na msimu huu wanaongoza ligi) ukiwa na kikosi B, huku ukiwategemea kina Crispine Ngushi, Mzize, na Jesus Moloko. Huo ni mzaha katika soka. Yanga wamejimaliza wenyewe.