IKIWA leo ni siku ya mwisho kwa dirisha dogo la usajili kufungwa klabu ya Yanga imetangaza kuwa inakamilisha usajili wake wa mwisho kwa kushusha mshambuliaji ambaye atakuja kuwasahulisha mashabiki aliyekuwa straika wao kipenzi, Fiston Mayele.
Tangu ameondoka Mayele, Yanga haijapata mbadala mwingine wa nyota huyo badala ya Hafiz Konkoni aliyesajiliwa kuwa mbadala wake kyshundwa kutendea haki nafasi hiyo, huku viungo wakiongoza kufumania nyavu za timu hiyo.
Rais wa Yanga, HersI Said amesema wanakamilisha usajili wa mshambuliaji mpya ambaye utafunga zoezi hilo kwa kutibu tatizo la safu ya ushambuliaji kulingana na mapendekezo ya kocha Gamondi (Miguel).
Amesema baada ya kufanikiwa kumtambulisha nyota wawilo wapya sasa mashabiki wakae mkao wa kutulia kwa sababu wako katika hatua za mwisho kushusha kifaa kipya kuimarisha kikosi cha timu yao katika safu ya ushambuliaji
“Licha ya ugumu kupata mshambuliaji mzuri kwa sasa kwa sababu ya wengi wao wako katika klabu zao lakini tumepambana na kuhakikisha tunafanikiwa kumsajili mtu ambaye atakuja kucheza na kusaidia timu kwenye safu ya Ushambuliaji.
Bado hatujapata mtu sahihi pale nyuma wa kutufungia hali ambayo Kocha wetu ametuhimiza kutafuta mshambuliaji ambaye atakuja kumaliza tatizo hilo katika kikosi cha timu yetu,” amesema Rais huyo wa Yanga.
Ameongeza kuwa kulingana na ugumu huo wamelazimka kuchukuwa muda mrefu kupata mshambuliaji kwa sababu akihitaji kujiridhisha na uwezo wake ili kusaidia timu kupata matokeo mazuri na kutetea mataji yao.
Amsisitiza kuwa msimu huu wanahitaji kuendeleza walipoishia msimu uliopita kutetea taji lao la ubingwa na kuweka rekodi nzuri, Kombe la FA na kucheza nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo msimu uliopita walicheza fainali ya Shirikisho.
Kuhusu baadhi ya nyota wawili anaotajwa kuhusishwa na Yanga, Sankara Karamoko,
Leonal Ateba wa Cameroon na Glody Kilangalanga, alisema katika usajili hayo yapo na kuwataka mashabiki kutulia kuona wanavyosajili.
Ameeleza kuwa Yanga wanauwezo wa kusajili vizuri anaimani kama walivyokuja kina Pacome Zouzoua, Aziz Ki Stephen ndio wachezaji wengine watatua ndani ya kikosi cha mabingwa hao watetezi wa ligi Bara.