Zoezi la Kutafuta Mwili wa Kijana Aliyejirusha Baharini Lafungwa Bila Mafanikio

Zoezi la Kutafuta Mwili wa Kijana Aliyejirusha Baharini Lafungwa Bila Mafanikio



Kikosi Maalum cha kuzuia Magendo KMKM leo kimekamilisha na kufunga zoezi la utafutaji wa mwili wa kijana Mahmoud Mwalim aliyejirusha kwenye bahari wakati akiwa katika boti ya Zanzibar 3 iliyokuwa inatokea Pemba kwenda Unguja

Akizungumza na Wasafi Media Mkuu wa Operesheni KMKM Zanzibar Captain Hussein Mohamed Seif amesema zoezi hilo liloanza Januari 21, mwaka huu ambapo limedumu kwa siku tatu huku leo likitamatishwa kwa kuongezwa nguvu ya ziada ya kutandaza boti za utafutaji katika maeneo mbalimbali

Aidha amesema zoezi hilo limefungwa bila ya mafanikio yoyote huku wakiendelea kuwaomba wananchi kutoa taarifa kwa mamlaka husika pindi watakapouona mwili huo

Amesema wanadhani mwili huo utakuwa umesogezwa ufukweni na maji hivyo ni vyema wananchi kutoa taarifa pindi watakapoona

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad