Akutwa na alama za Barabarani za Tsh milioni 10 ndani

Akutwa na alama za Barabarani za Tsh milioni 10 ndani


Jeshi la Polisi mkoani Tabora linamshikilia jamaa aliyefahamika kwa jina la Moshi, kwa tuhuma za uharibifu na wizi wa alama za usalama barabarani kutoka katika barabara mbalimbali katika mkoa huo baada ya kukutwa na alama zenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 10 nyumbani kwake.


Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari Kamanda wa Polisi, ACP Richard Abwao, amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa saa 12 asubuhi katika Kata ya Usege wilayani Kaliua.


Amesema walimkamata mtuhumiwa huyo baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema ambao wanapiga vita vitendo vya uharibifu wa alama za barabarani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad