Ally Kamwe: Simba vs Azam tunaomba watoke sare, Tuzidi Kuwapiga Gap

 

Ally Kamwe: Simba vs Azam tunaomba watoke sar

Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa anaomba dua mchezo wa leo kati ya Simba SC dhidi ya Azam FC umalizike kwa sare ili timu yao ishushe presha pale kwenye kilele cha msimamo wa Ligi hiyo.


Kamwe amesema hayo kuelekea mchezo huo utakaopigwa leo Ijumaa, Februari 9, 2024 katika Dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza.


“Kiukweli mechi ya Simba SC dhidi ya Azam Fc, mimi sina timu nitakayoishabikia, matokeo ninayoyataka pale ni sare, ikitokea Mungu ameamua mmoja afungwe, basi afungwe makolo.


“Mimi sitaki yeyote afungwe kabisa, lakini kama ni lazima mmoja afungwe, basi dua yangu nipate mtu wa kumcheka. Azam yupo Ibwe na Zaka, dua yangu ya kuwacheka imeshaisha, basi afungwe Kolo, nimcheke Ahmed Ally na wenzake, wako wengi,” amesema Kamwe.


Yanga wapo nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi hiyo wakiwa na alama 37, michezo 14, Azam FC nafasi ya pili, alama 31, michezo 13 na Simba nafasi ya tatu, alama 29 na michezo 12.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad